Njia 7 namna kuepuka kuingia kwenye madeni baada ya harusi

0
63

Sherehe ya harusi ni tukio la furaha na la kukumbukwa kwa kila mmoja, lakini mara tukio hilo linapokwisha mara nyingi wahusika hujikuta wakiingia kwenye madeni makubwa.

Wanandoa wanaweza kuepuka madeni ikiwa watapanga mikakati mizuri ya awali.

Hizi ni njia 7 zitakazokusaidia kufanikisha harusi yako bila kuingia kwenye madeni hayo;

Usiwe na haraka
Wanandoa wanaweza kuzuia gharama zisizo za lazima kwa kuchagua tarehe inayofaa ambayo itawaruhusu kupata pesa za kutosha. Wewe na mpenzi wako mnapaswa kuweka vichwa vyenu pamoja ili kuchagua tarehe ambayo itawawezesha kufikia malengo yenu ya kifedha.

Jadili na wanandoa wengine
Kuwasikiliza wanandoa wengine kunaweza kuwa na manufaa kwa sababu ya uzoefu wao wa kuandaa harusi. Wanaweza kuwa na ushauri muhimu wa kutoa kuhusu kile kilichotokea wakati wa harusi yao na jinsi unavyoweza kuepuka kufanya makosa fulani.

Aina 5 za magari yanayotumia mafuta mengi zaidi

Anza kuweka akiba
Ikiwa una mpango wa kuoa na hutaki kuingia kwenye madeni, anza kuweka akiba. Ni vyema kuanza kuweka akiba miezi au miaka kadhaa kabla ya harusi yako ili usilemewe na gharama unazoweza kutumia katika kipindi hicho.

Tengeneza bajeti
Kuwa na bajeti ni mojawapo ya njia bora ili kuepuka madeni. Unaweza kutumia zaidi ya ilivyotarajiwa ikiwa huna bajeti. Chora makadirio na jumla ya pesa utakayotumia, kisha gawa pesa kwa kila gharama na kila jambo hata kama ni kitu kisicho na muhimu sana.

Zungumza na familia yako
Kuhusisha familia yako ni mojawapo ya mikakati bora ya kuzingatia. Unaweza kuwaambia baadhi ya wanafamilia wako kukusaidia gharama fulani badala ya kukupa zawadi.

Usialike watu wengi
Kualika watu wengi itakulazimu kutafuta ukumbi mkubwa, chakula zaidi, vinywaji, nk. Kwa hivyo, zingatia zaidi watu ambao ni muhimu zaidi katika maisha yako badala ya kualika kila mtu.

Omba msaada kwa marafiki
Wewe na mwenzi wako mnaweza kuwahusisha marafiki zenu wa karibu ili kupata usaidizi. Baadhi yao wanaweza wasikuunge mkono kwa hali ya kifedha, lakini wanaweza kusaidia katika kuifanya siku yako kuwa ya kukumbukwa.

Send this to a friend