Njia 7 za kutambua kama iPhone ni feki

0
69

Kwa sababu simu zilizoghushiwa mara nyingi kwa mwonekano wa nje hufanana na simu halisi, huwa ni vigumu sana kutambua kwa kuangalia kwamba simu hii ni halisi na hii ni feki.

Kutokana na ugumu huo, watu wengi wamekuwa wakiuziwa simu feki kwa kuaminishwa kwamba ni halisi, lakini wengine wamekuwa wakiuziwa simu zilizotumika wakiaminishwa kwamba ni mpya.

Katika teknolojia leo tutakupitisha hatua kwa hatua kwenye njia za kuweza kubaini kama simu ya iPhone ni halisi au feki. Kunaweza kuwepo kwa njia nyingine zaidi ya tutakazoziangazia, tumia zote kujiridhisha kabla ya kufanya manunuzi.

1. Angalia mpangilio wa boksi.
Sharti simu mpya ije ikiwa kwenye boksi lake ambapo lazima lioneshe namba ya toleo (model number), nambari ya utambulisho (serial number) na IMEI. Namba zote hizi lazima zilandane na zinazoonekana kwenye simu yake kwa kufungua Setting > General > About. Kama hazifanani, simu hiyo ni ya kutia walakini.

Simu 5 salama zaidi kutumia duniani

2. Thibitisha namba ya utambulisho (serial number) kupitia https://checkcoverage.apple.com
Ingiza namba ya utambulisho katika kiungio hicho (Apple’s warranty status website), na utatakiwa kuona toleo, kipindi cha udhamini (warranty), support status na taarifa nyinginezo kuhusu simu. Ukiona ujumbe unaoeleza kuwa “We’re sorry, but this serial number is not valid,” kuna uwezekano kuwa simu yako si halisi.

3. Angalia nambari ya IMEI katika http://www.imeipro.info
Kila simu ina namba ya IMEI ambayo haifanani na simu nyingine. Kama IMEI namba ya simu yako inaonesha taarifa tofauti na za simu yake, basi ni wazi hiyo simu si halisi.

Kupata imei ya simu piga *#06#.

4. Sehemu ya kuweka ‘memory card’
Hakuna iPhone yenye sehemu ya kuweka memory card. Haijalishi simu hiyo itafananaje na iPhone, lakini kama ina sehemu ya memory card, tambua wazi sio kwamba ni iPhone bandia, bali sio iPhone kabisa.

5. Logo ya Apple
iPhone zote zina logo ye Apple, na haupaswi kuhisi utofauti, ama imepanda juu au mguso wake uwe tofauti na sehemu nyingine ya simu. Kama ukigusa hiyo logo unahisi utofauti na ukigusa sehemu nyingine ya nyuma ya simu, ni wazi kwamba si halisi.

iPhone 13 Pro yadukuliwa na wadukuzi wa China

6. Linganisha simu yako na iPhone nyingine iliyothibitika kuwa halisi
Zishike zote sambamba na kw akila unachofungua hakikisha zote zinaonesha sawa kuanzia taarifa hadi mwonekano. Kukiwa na utofauti wa simu unayotaka kununua au uliyo nayo, basi tambua kwamba si halisi. Unaweza kutumia kiungio hichi kukamilisha zoezi hilo, https://www.wikihow.com/Identify-if-Your-Phone-Is-an-Original-or-a-Clone#:~:text=https%3A//support.apple.com/en-us/HT201296.

7. Angalia App za msingi
Kuna programu tumishi ambazo utazipakua wewe, lakini kuna zile ambazo huja na simu kama vile App Store, Settings, Compass na Safari. Zikikosekana hizo, au ukiona nyinginezo kama Play Store, ni wazi kuwa unatumia Android yenye mwonekano wa iPhone.

Pia unaweza kufungua setting app kuangalia vitu kama Control Center, Siri & Search, na iTunes & App Store.

Send this to a friend