Nyama ya Tanzania kuanza kuuzwa nchini Misri

0
54

Nyama ya Tanzania inatarajia kuanza kuuzwa nchini Misri kabla ya sikukuu ya Eid al Hajj ambapo takribani tani 100 zinatarajia kusafirishwa ili kutangaza soko la Tanzania.

Hayo yameeelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Huduma za Miradi ya Misri (NSPO), Meja Jenerali Hossam Nigeda baada ya kukutana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega jijini Dodoma ambapo amesema lengo lao ni kuendelea kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili kwa kufungua soko la nyama ya Tanzania nchini humo.

Tanzania yakusanya bilioni 70 kwa ndege zinazotumia anga lake

Aidha, Jenerali Nigeda amesema wamejipanga kuanzisha machinjio ya kisasa nchini Tanzania ambayo itawezesha kusafirisha tani 600 ya nyama kila mwezi pamoja na kusafirisha wanyama hao wakiwemo ng’ombe, kondoo na mbuzi 10,000 kila mwezi.

Kwa upande wake Waziri Ulega amesema Misri ni miongoni mwa nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, hivyo kufanyika kwa biashara hiyo ni fursa nzuri katika uchumi wa Tanzania, na amemhakikishia kuwa Tanzania iko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha biashara hiyo.

Send this to a friend