Nyaraka za ujenzi wa madarasa Mtama hazijulikani zilipo

0
50

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Sahili Geraruma amekataa kuzindua madarasa manne yaliyojengwa  kwa fedha za maendeleo zilizotolewa na Serikali  katika shule ya sekondari  Madangwa, Halmashauri ya Mtama Mkoa wa Lindi.

Amesema amekataa kuzindua ujenzi huo kwa sababu ya kasoro nyingi zilizoonekana, ikiwemo kukosekana kwa ubora wa madawati licha ya shilingi milioni 84 kutolewa shuleni hapo, na kuongeza kuwa nyaraka nyingi kuhusu mradi huo hazionekani.

“Fedha hizo zimetolewa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha watoto wetu wanasoma katika madarasa mazuri, hivyo niwaombe viongozi wa Serikali msimamie kikamilifu miradi bila kuleta janja janja yoyote,” amesema Geraruma.

Aidha, amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Lindi kuhakikisha anafuatilia kwa kina nyaraka zote za mradi huo.

Send this to a friend