Nyaraka Zavuja: Mabilioni ya umma DRC yalitoroshwa Rais Kabila akiwa madarakani

0
12

Nyaraka zilizovuja zimeonesha kuwa mabilioni ya fedha umma yalitoroshwa nchini DR Congo na Kampuni zilizomilikiwa na familia na marafiki wa Rais Msstaafu, Joseph Kabila.

Skendo hiyo kubwa Afrika inaeleza kuwa  fedha zilitoroshwa kupitia tawi laa Benki ya BGFI (Banque Gabonaise et Française Internationale) nchini humo ambayo dada wa Rais Kabila, Gloria Mteyu alikuwa anamiliki 40% ya benki hiyo.

Nyaraka hizo zaidi ya milioni 3 zinaonesha baada ya muda fedha taslimu zilitolewa kwenye akaunti hizo, lakini bado haijafahamika ni nani alinufaika na fedha hizo, na kama kuna mgongano wa kimaslahi.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa BGFI kutoka mwaka 2012 hadi 2018 ni Francis Selemani ambaye alilelewa na wazazi wa Rais Kabila.

Katika taarifa iliyochapishwa mitandaoni, Rais Kabila amekanusha madai hayo na kusema ni shutuma zisizo na msingi.

Send this to a friend