Nyongeza ya mishahara kuanza Julai 2022

0
49

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara ya watumishi kutoka kwa timu ya wataalamu iliyokuwa ikiyaandaa kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amepokea taarifa hiyo Mei 10, 2022 katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma kikiwahusisha viongozi wa wizara mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema taarifa hiyo imeonesha kwamba maandalizi ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara yameshakamilika na kwamba wakati wowote atayawasilisha kwa Rais ambaye atautangazia umma mabadiliko hayo yanayotarajiwa Julai mwaka huu.

Rais wakati akihutubia wananchi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi 2022) aliwahikikishia wafanyakazi nchini kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 itaongeza mishahara kwa watumishi wake.

Send this to a friend