Nyota wa MTV afariki baada ya kufanya ‘plastic surgery’

0
43

Ripoti ya Mkaguzi wa Matibabu nchini Marekani imebainisha kuwa kifo cha nyota wa MTV na mwigizaji, Jacky Oh (33) aliyefariki Mei 31 mwaka huu kimetokana na upasuaji wa kuboresha umbo (plastic surgery).

Mwakilishi wa Idara ya Polisi ya Miami ameweka wazi kwamba idara hiyo haitamtia hatiani daktari aliyemfanyia upasuaji na kuita kwamba ni “ajali inayotokana na matatizo yanayohusiana na upasuaji wa masuala ya urembo”.

Aidha, ripoti hiyo inaeleza Jacky ambaye ni mama wa watoto watatu alisafiri kutoka Georgia hadi Florida kwa ajili ya upasuaji uliofanyika Mei 30, mwaka huu ambapo daktari wake alimwandikia kutumia ciprofloxacin na oxycodone za kutuliza maumivu pamoja na dawa ya kuzuia kichefuchefu ‘odansetron’.

Utata waibuka baada ya Zimbabwe kupata miss ‘mzungu’

Hata hivyo, imeelezwa kuwa alianza kupata maumivu ya kichwa baada ya upasuaji, na muuguzi akamshauri kuacha kutumia odansetron na kuchukua ibuprofen ambapo hatua hiyo haikufanya kazi mpaka kupelekea kushindwa kuongea hadi kifo chake.

Jacky Oh ambaye jina lake halisi ni Jacklyn Smith alikuwa sehemu ya mchezo maarufu  wa vichekesho wa Wild N’ Out nchini Marekani.

Send this to a friend