Odinga: Tutafanya maandamano kila Jumatatu

0
23

Kiongozi wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza kwamba kutakuwa na maandamano ya kile alichokiita kupigania haki ya Wakenya kila Jumatatu mpaka gharama za vyakula zitakaposhuka.

Akihutubia waandamanaji kwenye msafara wake alipojiunga nao katika eneo la Eastleigh Nairobi, Odinga amesema maandamano yaliyofanyika leo Jumatatu ulikuwa ni mwanzo tu wa kile walichokianzisha.

“Leo tumekuwa na maandamano town (mjini), Jumatatu Wakenya watakuwa na maandamano ya kiamani. Wameshikwa na uwoga lakini tutaendelea mpaka bei ya unga irudi chini.

Waandamanaji Kenya watawanywa kwa mabomu ya machozi

Kila Jumatatau kutakuwa na mgomo, kutakuwa na maandamano. Vita imeanza na haitaisha mpaka Wakenya wapate haki yao,” amesema.

Raila Odinga ameandamana na aliyekuwa mgombea mwenza katika uchaguzi uliopita, Martha Karua na wanasiasa wengine wa upinzani ambao walimuunga mkono.

Odinga amesema kujitokeza kwa watu katika maandamano ya leo Jumatatu ni ishara kuwa Wakenya wamechoshwa na uongozi uliopo madarakani chini ya Rais William Ruto.

Send this to a friend