Ofisi mpya kujengwa Ikulu ya Chamwino, Dodoma

0
86

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekagua maandalizi ya sherehe za uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma zitakazofanyika kesho 30 Mei 2020.

Jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi hizo litawekwa na Rais Dkt. Magufuli, Mama Maria
Nyerere (kwa niaba ya Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere), Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Dkt. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu. Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi.

Send this to a friend