Ofisi ya Msajili: Mbatia asijihusishe na siasa

0
40

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imemsimamisha James Mbatia na sekretarieti yake yote kutojihusisha na siasa ndani ya chama cha NCCR Mageuzi mpaka atakapojitetea katika mkutano mkuu wa chama hicho.

Msajili msaidizi wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza amesema wamejiridhisha baada ya kupitia nyaraka zilizowasilishwa na chama, hivyo wanamuomba Mbatia kutojishughulisha na shughuli za chama.

Uamuzi huo umekuja baada ya halmashauri kuu ya chama hicho kumsimamisha Mbatia na Makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtaigwa kutojishughulisha na shughuli zozote za chama hicho mpaka watakapoitwa kujitetea kwenye mkutano mkuu.

Hata hivyo Mbatia na wenzake hawakukubaliana na maamuzi hayo ya kusimamishwa uanachama yaliyofanyika Mei 21 mwaka huu wakituhumiwa kukosa uaminifu.

Send this to a friend