Viongozi wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) wametembelea Mradi wa Kimkakati wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) na kuipongeza Serikali kwa usimamizi wa mradi huo utakaozalisha megawati 2,115 kuanzia Juni, 2024, baada ya ujenzi wake kukamilika.
Viongozi wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) wakisikiliza maelezo ya maendeleo ya mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) kabla ya kuanza kutembelea maeneo mbambali ya ujenzi wa mradi huo.
Waziri wa Nishati, January Makamba (Katikati),Kaimu Mufti Shekh Ally Khamis Ngeruko, kutoka Baraza kuu la Waislam Tanzania ( wa pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (wa pili kulia), Naibu Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiisalam Tanzania, Bi.Khanifa Mahamud Karamagi (wa kwanza kulia), wakiwa na wengine viongozi wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Waziri wa Nishati, January Makamba (Katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) pamoja na watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Waziri wa Nishati, January Makamba akizungumza jambo wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere iliyofanywa na viongozi kutoka Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Julai 12, 2023.
.Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere iliyofanywa na Viongozi kutoka Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA).
Waziri wa Nishati, January Makamba (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati), Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Innocent Luoga, wakizungumza jambo wakati wa ziara ya kutoka Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA).