Ommy Dimpoz afunguka ukaribu wake na Diamond

0
71

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo maarufu kama ‘Ommy Dimpoz’ amesema kwamba msanii mwenzake Diamond Platnumz hakuhusika na tatizo lake la kiafya ambalo lilimuathiri kwa kiasi kikubwa na kupelekea kukaa hospitali kwa muda mrefu.

Ommy Dimpoz ameyasema hayo baada ya kuonekana kuwa karibu na Diamond Platnumz jambo lililozua maswali kwa watu baada ya wawili hao kutokuwa na ukaribu kwa muda mrefu.

Msanii aitaka kampuni ya mabasi imlipe milioni 123 kwa kutumia wimbo wake

“Namshukuru Mungu kwa kuwa na afya, lakini tatizo langu la kiafya halikuhusiana na mtu yeyote ilikuwa tu ni mambo ya Mungu,“ amesema Ommy Dimpoz katika mahojiano na kituo cha televisheni cha EATV.

Ommy Dimpoz alilazwa nchini Afrika Kusini baada ya kufanyiwa upasuaji wa koo kutokana na kile kilichosemwa na watalaam kuwa alikula kitu chenya sumu.

Send this to a friend