Ongezeko la mahitaji, ukame, matengenezo vyachangia upungufu wa umeme nchini

0
50

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Gissima Nyamo-Hanga amesema shirika limeweka mikakati kuhakikisha kuwa kufikia mwishoni mwa Machi 2024, tatizo la kukatika kwa umeme linamalizika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, amesema kiwango cha upungufu cha megawati 400 katika vituo vya uzalishaji umeme nchini kilichochangiwa na ongezeko la mahitaji ya umeme kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi, upungufu wa maji kwenye vituo vya kufua umeme unaotakana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na matengenezo ya mitambo yanayoendelea, kinatarajiwa kupungwa ili kutatua tatizo hilo.

“Matarajio yetu ni kwamba hiki kiwango cha upungufu cha megawati 400 tutakuwa tunakipunguza polepole na tunatarajia ndani ya wiki mbili tatizo hili litaanza kupungua makali na mpango tulionao ni wa kuendelea kulipunguza kwa wastani wa megawati 100 kwa kila mwezi kwa maana kwamba tunatarajia mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi wa tatu tatizo hili liwe limekamilika kabisa,” amesema.

TIC: Thamani y auwekezaji nchini yapanda kwa asilimia 120

Aidha, amesema shirika linaendelea kukamilisha utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere litakalokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2115 ambao mpaka sasa umefikia asilimia 92 na pindi mradi huo utakapokamilika na kuingizwa kwenye gridi ya taifa, utachangia kuimarika kwa hali ya umeme nchini kwa kiasi kikubwa.

Send this to a friend