Onyo la polisi kwa wanaotorosha mifugo nje ya nchi

0
45

Kamanda wa Kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo Tanzania, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Simon Pasua ametangaza kiama kwa watoroshaji wa mifugo nje ya nchi.

Pasua amesema hayo leo Juni 06, 2022 wakati akizungumza na askari wa kikosi hicho jijini Arusha na kueleza kuwa zipo taarifa za watu wachache wanajihusisha na utoroshaji wa mifugo nje ya nchi.

Aidha, amewataka watendaji wa kikosi hicho kutojihusisha kwa namna yeyote na watuhumiwa wenye lengo la kutorosha mifugo, amesema kwani kwa kufanya hivyo kutapunguza pato la Taifa.

Kisa kulewa haraka, TMDA kuchunguza vilevi vinavyowekwa kwenye shisha

Amewataka pia wafugaji kote nchini kufuata taratibu za uuzaji wa mifugo yao ili kuongeza pato la Taifa kwa ujumla.

Send this to a friend