Operesheni kukamata wanaotumia mifuko ya plastiki yatangazwa

0
36

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ametangaza operesheni ya kukamata mifuko ya plastiki iliyokatazwa nchini na kuwataka wananchi kujiepusha na matumizi ya mifuko hiyo.

Ameagiza kuitishwa kikao cha wenyeviti wa masoko yote ya mkoa huo na kutolewa maelekezo ya katazo la uuzaji wa mifuko iliyokatazwa kwenye masoko yao.

Pamoja na hayo, Makalla ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Mazingira NEMC kutoa elimu upya kwa wananchi kuhusu madhara ya matumizi ya mifuko hiyo.

Agizo la Dkt. Mpango kwa Jeshi la Polisi

Miongoni mwa madhara ya matumizi ya mifuko iliyokatazwa ni uchafuzi wa mazingira, ukwepaji wa kodi kutokana na mifuko kuuzwa kinyemela pamoja na kuua viwanda vilivyopewa kazi ya kuzalisha mifuko mbadala.

Kwa upande wao NEMC na TBS wametumia kikao hicho kutoa tamko la kusimamia operesheni hiyo ambapo wamemuahidi Mkuu wa Mkoa kuwa Operesheni hiyo itafanikiwa.

Send this to a friend