Orodha mpya: Akaunti 25 za ku-follow Twitter Tanzania (ToT) mwaka huu wa 2019

0
52

Mtandao wa Twitter ni moja ya sehemu zinazoongoza kwa mijadala mikubwa mtandaoni nchini Tanzania kwa sasa, na hata kwa burudani, vijembe, ngebe, na ubabe pia.

Twitter Tanzania pia ni sehemu yenye viongozi wengi zaidi wa serikali, wasanii na watu wengine mashuhuri labda kuliko mtandao mwingine wowote ule.

Hapa chini tunazitazama akaunti 25 ambazo kwa kuzi-follow zitaweza kuyafanya matumizi yako ya mtandao wa Twitter kuwa angavu zaidi. Uchaguzi wa akaunti hizi umetazama aina ya maudhui, wakati mwingine idadi ya followers, na msambao wa kile kinachobandikwa kwenye akaunti hizo mara kwa mara.

25

@MarekaMalili

Hapo utapata mara nyingi retweets au tweets za nini kinajadiliwa kwa kiasi kikubwa Twitter siku hiyo. Iwe ni mtu anauza bidhaa, au mgonjwa anahitaji msaada au tamasha.

24

@DannyMsiriz

Huyu jamaa ni mpiga picha lakini na hawa wapo wengi Twitter ila jicho lake na ujuzi wake kwenye picha ni wa kipekee hasa picha za maeneo mbalimbali anayotembelea. Hutajutia kum-follow.

23

@Wakazi

Labda msanii pekee ambaye yuko huru sana kueleza anachojisikia kueleza. Huwa hatweet mara nyingi lakini akitweet yuko huru.

22

@Joti

Joti ni Joti, hamna maelezo.

21
@allysalehznz

Mwanasheria, Mbunge wa Malindi, Mwanahabari, Mshairi. Labda akaunti pekee ya ku-follow ukitaka kujua Kiswahili fasaha. Ally anajadili siasa, utaifa, sheria na wakati mwingine utani.

20

@TonyTogolani

Yeye huwa ana nasaha ambazo zinatokana na maisha yake na uzoefu wake wa kila siku. Tweet zake za Sikiliza Togolani ni sawa na kusema sikiliza mtu yeyote yule. Mimi huwa nampenda yule mshauri wake wa masuala ya kipumbafu.

19

@Abbymexahnk

Huyu huwa anatoa hints hasa kwa wale wanaotafuta ajira.

18

@givenality

Ideas hasa kwenye technology. He might not be the guru kwenye technology hapo ToT ila ana hints za hapa na pale zinaweza kukupa some constructive thoughts.

17

@mxcarter

Mapicha sana sana. Jamaa anasafiri sehemu mbalimbali na events kwa hiyo na wewe unasafiri kwa jicho.

16

@salim_alkhasas

Pia anaitwa Papaa Mchoyo, mutu ya Roho Mbaya. Kwa kweli hii akaunti kuna kila kila kitu. Ngebe, points, charity, fitna, soccer, ujasiriamali, KILA KITU. Na majibu ya shombo sometimes.

15

@JaliluZaid

Mpiga picha, anaibukia. He’s a humble kid. Ndevu hana, can make a cool radio presenter ana sauti ya kazi hiyo but maybe vyeti hana au connection.

14

Salama Jabir @Ecejay

Salama ni Salama. Burudani, maisha, sometimes ibada na haogopi kukujibu inavyotakiwa ukimchefua. Siku hizi anatangaza mpira DSTV.

13

@HKigwangallah

Labda Waziri peke yake ambaye mnaweza kubishana hadi mkafikia mwisho kwenye issue hapo hapo Twitter. Ana ngozi ngumu na subira maana mimi ningekuwa Level zake unitukane Twitter sikuachi hivi hivi, nakutafuta mtaani nakuweka Sawa, I think that’s why Mungu hanipi madaraka.

12

@Tanganyikan

Huyu ni mmoja ya watu wa mwanzo kabisa kujenga hii spirit ya ToT. Mkongwe wa Twitter pia na anatoa support kwa watu mtandaoni hapa na pale so ni account nzuri to follow.

11

@Fatma_Karume

Wakili, aliwahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika. Dada anajiamini huyu hadi mimi naogopa kwa niaba yake. Huwa namfolo sababu yuko huru sana na haogopi kusema anachoamini.

10

@moodewji

Maisha, ibada, fitness, biashara, mpira. Mshua anayeelewa namna ya kuwa mshua halafu kazaliwa ushuani. Pia kama unataka kusikia exclusive za Simba SC, mfollow ila kama shabiki wa Yanga zile post zake za nyasi za Simba Bunju na usjali utakuwa unaumia tu.

9

@Chahali

Chahali ni Chahali. Anaishi Uskochi ila Mbongo tu. Mfollow kwa ajili ya mengi sana kama uchumi, ushushushu na kadhalika. Ukimzingua anakupiga tofali fasta.

8

@Benji_Fernandes

The kid is just inspirational man. Kuna siku kasema Bill Gates alimpa kazi akakataa. Sasa huwezi kujua siku anaweza hata kugawa vocha Twitter. Mimi namfolo sababu naona ana mengi ya mtu kujifunza hata katika utu uzima huu. Elimu haina mwisho.

7

@mkandamizaji

Mkandamizaji ni Mkandamizaji. Siku hizi kaoa kwa hiyo kuna mambo hatweet tena, na kawa mchungaji. Ila bado ana tweets nzuri sometimes za utani na kuchekesha.

6

@MasoudKipanya

Modern day philosopher hivi na vikatuni vyake vile vya Kipanya

5

@MariaSTsehai

I think Maria retweets almost everything significant for the day. So she is like my twitter summary except jokes hamna.

4

@ZittoKabwe

Zitto ni Zitto. Siasa, ubishi wa kitabu, mara kakamatwa kahojiwa, uchumi, etc. sasa hivi Twitter wameiondoa account yake hewani sijui kwa nini.

3

@JMakamba

Ngumu kuelewa tweets zake sometimes lakini kiongozi anayejiachia vizuri na tweeps na mijadala inakwenda vizuri. Siku hizi wanamuita Twitter darling, toka aondolewe cabinet naona kama kapunguza ku-tweet. Poetic, smart, and smartly sarcastic sometimes. Ila kuna watu walishachezea tofali zake.

2
@jmkikwete

Still the best place kupata mbili tatu za Mstaafu, kama zile picha zake akiwa anavuna mahindi au kugawa madafu kwa kuku na kula ugali na ndugu zake msibani Msoga. I mean imagine without Twitter tungejuaje huwa anakaa chini kula ndugu zake msibani? Maana ukishastaafu hupati sana airtime kwenye mainstream, mfano I wish ningekuwa napata updates za Mkapa. I like him most.

1
@MagufuliJP

Ndo mwenye nchi. Sasa utajuaje siku ambayo ametweet leo hakuna kutweet? Tweets zake zinahesabika, shows up when kuna issue kubwa sana, anatupia tweet anawaacha muhangaike nayo anaenda zake.

Na mimi basi mnifollow jama @nyamokomayagilo

Send this to a friend