Orodha ya filamu 10 bora za mwaka 2022

0
53

Ikiwa wewe ni mpenzi na mfuatiliaji wa filamu, utakuwa na orodha ya baadhi ya filamu zilizotoka mwaka huu zinazofanya vizuri.

Endapo bado hujui ni filamu ipi nzuri ya kuangalia hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka, fuatilia orodha hii ya filamu 10 bora kwa mujibu wa wachambuzi wa BBC.

1. Turning Red
Turning Red imeongozwa na Domee Shi. Filamu inamhusu mwanafunzi wa Kichina mwenye umri wa miaka 13 ambaye kwa sababu ya laana ya urithi, anabadilika na kuwa panda mkubwa mwekundu kila anapopata hisia kali.

2. Everything Everywhere All at Once
Ni filamu ya Kimarekani ya 2022 inayomhusu mhamiaji wa Kichina anayejiingiza katika matukio ya kusisimua bila kupenda ambapo lazima ajiunganishe katika aina ya ulimwengu fulani ili kumzuia mtu ambaye ana nia ya kudhuru watu.

3. Top Gun: Maverick
Baada ya zaidi ya miaka 30 ya utumishi kama mmoja wa waendeshaji ndege wakuu wa Jeshi la wanamaji, Maverick anakabiliana na maisha yake ya zamani alipokuwa akitoa mafunzo kwenye kikundi cha wahitimu wadogo wa Top Gun akiwemo mtoto wa rafiki yake mkubwa aliyekufa kwenye misheni hatari.

4. After Yang
Wakati roboti mpendwa wa binti yao mdogo Jake na Kyra inapoharibika, Jake anatafuta njia ya kuirekebisha. Katika mchakato huo, Jake anagundua maisha ambayo yamekuwa yakipita mbele yake anapoungana tena na mkewe na binti yake. Filamu hii imeandikwa, kuongozwa, na kuhaririwa na Kogonada.

5. The Eternal Daughter
Msanii na mama yake mzee wanakabiliana na siri zilizozikwa kwa muda mrefu katika nyumba yao ya zamani ya familia ambayo sasa ni hoteli inayoandamwa na siku na mambo ya ajabu. Imeandikwa, kutayarishwa na kuongozwa na Joanna Hogg.

6. Doctor Strange in the Multiverse of Madness
Baada ya kupata ndoto mbaya kila usiku, Doctor Strange anaungana na msichana wa ajabu kutoka katika ndoto zake ili kupambana na vitisho vingi vinavyotishia kuangamiza mamilioni ya watu. Filamu hii ni muendelezo wa Doctor Strange (2016).

7. Tár
Tár ni filamu iliyoandikwa na kuongozwa na Todd Field na kuigiza na Cate Blanchett. Filamu hii inaelezea kuinuka na kuanguka kwa mtunzi mashuhuri wa muziki Lydia Tár.

8. The Fabelmans
Kijana Sammy Fabelman anapenda sinema baada ya wazazi wake kumpeleka kuona “The Greatest Show on Earth.” Akiwa na kamera, Sammy anaanza kutengeneza filamu zake mwenyewe nyumbani, jambo ambalo linamfurahisha mama yake.

9. RRR
Mwanamapinduzi asiye na woga na Afisa katika jeshi la Uingereza ambaye anaamua kuunganisha nguvu na kutafuta uhuru dhidi ya watawala wa Kimabavu.

10. Happening
Mnamo 1963, mwanafunzi Anne ambaye ana mustakabali mzuri mbele yake, ndoto zake za kumaliza masomo yake inakatizwa baada ya kupata ujauzito. Anne anaamua kukabiliana na aibu na uchungu wa kutoa mimba, hata ikiwa ni lazima ahatarishe kifungo kufanya hivyo.

Send this to a friend