Orodha ya maafisa wa JWTZ waliopandishwa vyeo na Rais Magufuli
Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Magufuli wamewapandisha vyeo maafisa wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuwa brigedia jenerali na wengine kuwa meja jenerali.
Waliopandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kanali (Balozi) Wilbert Ibuge na Kamishna wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Kanali Francis Mbindi.
Waliopandishwa cheo kuwa Meja Jenerali ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Brigedia Jenerali Suleiman Mzee, Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari ya Dawa (MSD), Brigedia Jenerali Gabriel Mhidze.
Wengine ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali Charles Mbunge na Mkuu wa Chuo cha Maafisa Monduli, Brigedia Jenerali, Ibrahim Mhona.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Luteni Kanali Gaudentius Ilonda, maafisa hao wamepandishwa vyeo kuanzia Juni 2, 2020.