Orodha ya mabilionea barani Afrika. Utajiri wa MO Dewji wapungua

0
64

Mlipuko wa janga la Ugonjwa wa  Virusi vya Korona (UVIKO19) liliathiri baadhi ya biashara huku kwa upande mwingine likikuza biashara hasa zinazofanyika kwa njia ya mtandao na huduma za mawasiliano.

Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, mabilionea wa Afrika waliingiza $84.9 bilioni (TZS trilioni 196) ikiwa ni ongezeko la asilimia 15 zaidi ya utajiri wao.

Jarida la Forbes limetoa orodha ya mabilionea wa Afrika ambapo Afrika Kusini na Misri ndio mataifa yenye mabilionea wengi, nchi zote mbili zikiwa na mabilionea watano kila mmoja zikifuatiwa na Nigeria yenye mabilionea watatu.

Katika Orodha hiyo , bilionea Aliko Dangote aliongoza kwa mara nyengine barani Afrika akiwa na utajiri wa thamani ya $13.9b (TZS trilioni 32.1).

Katika nafasi ya pili ni bilionea wa Afrika Kusini, Johann Rupert ambaye alipanda kutoka nafasi ya nne mwaka jana.

Kutoka Tanzania bilionea kwenye orodha hiyo ni Mohammed Dewji, ambaye utajiri wake ulipungua hadi wastani wa dola bilioni 1.5 (TZS trilioni 3.5) kutoka dola bilioni 1.6 ( (TZS trilioni 3.7) mwaka mmoja uliopita.

Mwanamke wa mwisho kuorodheshwa miongoni mwa matajiri hao ni Isabel Dos santos wa Angola ambaye aliondolewa katika orodha hiyo ya watu matajiri Januari 2021.

Hapa chini ni orodha kamili ya mabilionea hao;

1. Aliko Dangote $13.9b

2. Johann Rupert & family $11b

3. Nicky Oppenheimer & family$8.7b

4. Nassef Sawiris $8.6b

5. Abdulsamad Rabiu $7B

6. Mike Adenuga $6.7b

7. Issad Rebrab & family $5.1b

8. Naguib Sawiris $3.4b

9. Patrice Motsepe $3.1b

10. Koos Bekker $2.7b

10. Strive Masiyiwa $2.7b

12. Mohamed Mansour $2.5b

13. Aziz Akhannouch & family $2.2b

14. Michiel Le Roux $1.7b

15. Othman Benjelloun & family $1.5b

15. Mohammed Dewji$1.5b

15.Youssef Mansour$1.5b

18.Yasseen Mansour$1.1b

Send this to a friend