Orodha ya madaktari wapya 610 na vituo walivyopangiwa

0
38

Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeeleza kuwa zoezi la uchambuzi wa maombi ya kazi za udaktari yaliyopokelewa kuanzia tarehe 24 Machi, 2020 hadi tarehe 10 Aprili, 2020 limekamilika, na kwamba waliokidhi vigezo wamepangiwa kazi.

Kwa wote waliopangiwa, wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi kuanzia tarehe 11 Mei, 2020 hadi 25 Mei, 2020, watakaoshindwa kuripoti bila ya taarifa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa haraka iwezekanavyo.

Pia wametakiwa kuwasilisha kwa waajiri wao (Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa) vyeti halisi (Originals Certificates) kwa ajili ya kuhakikiwa na waajiri kabla ya kupewa barua za ajira. Vyeti hivyo ni kama ifuatavyo:
i) Cheti cha kuzaliwa;
ii) Cheti cha Kidato cha Nne na Sita/Diploma;
iii) Cheti cha kuhitimu Shahada ya Udaktari;
iv) Cheti cha Usajili wa Baraza la Madaktari Tanzania (MCT); na
v) Uthibitisho wa kumaliza Mazoezi kwa Vitendo (Internship).

Kwa Madaktari waliosoma nje ya nchi wametakiwa kuwasilisha vyeti vya ithibati (Accreditation Certificates) kutoka NACTE/TCU.

Hapa chini ni orodha ya madaktari hao waliopangiwa vituo vya kazi;

Send this to a friend