Orodha ya majina ya vijana 812 waliochaguliwa kujiunga na programu ya kilimo (BBT)

0
86

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametangaza awamu ya kwanza ya majina ya vijana 812 waliochaguliwa kujiunga na programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) watakaoanza mafunzo yao kwa kipindi cha miezi minne kuanzia Machi 17, mwaka huu.

Waziri Bashe amesema jumla ya maombi yaliyowasilishwa wizarani ni 20,227.

“Baada ya mafunzo yao, Wizara inaenda kuwakabidhi mashamba, na tutawakabidhi mashamba ambayo tayari yameshaandaliwa, na Mheshimiwa Rais [Samia Suluhu] tarehe 20 mwezi wa tatu atazindua ‘block farm’ ya kwanza. Wakati wanaendelea kusoma kile kipindi cha miezi minne sisi tunaendelea na ujenzi wa eneo la Membe la ekari 8,000 ili wakitoka kule wanaenda moja kwa moja shambani,” amesema.

Orodha ya majina ya vijana 812 waliochaguliwa kujiunga na programu ya kilimo (BBT)