Orodha ya Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa leo

0
40

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 5, 2020 amekamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi wa leo, Rais Magufuli amewateua Mawaziri 21 ambao wataungana na Mawaziri 2 walioteuliwa tarehe 13 Novemba, 2020, na amewateua Naibu Mawaziri 23.

Aidha, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wabunge 2 ambao pia amewateua kuwa Mawaziri.

Pia, Rais Magufuli ameongeza wizara mpya 1 ambayo ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Mawaziri walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

  1. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Elias John Kwandikwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
  2. Rais Magufuli amemteua Kept. Mst. George Huruma Mkuchika kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).
  3. Rais Magufuli amemteua William Vangimembe Lukuvi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
  4. Rais Magufuli amemteua Jumaa Hamidu Aweso kuwa Waziri wa Maji.
  5. Rais Magufuli amemteua Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  6. Rais Magufuli amemteua Jenister Joakim Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
  7. Rais Magufuli amemteua Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) aliyekuwa akishughulikia Afya, pia ameteuliwa na Mhe. Rais Magufuli kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  1. Rais Magufuli amemteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji)
  2. Rais Magufuli amemteua Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
  3. Rais Magufuli amemteua Prof. Joyce Lazaro Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
  4. Rais Magufuli amemteua Mashimba Mashauri Ndaki kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
  5. Rais Magufuli amemteua Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
  6. Rais Magufuli amemteua Selemani Saidi Jafo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).
  7. Rais Magufuli amemteua Dkt. Medard Matogolo Kalemani kuwa Waziri wa Nishati.
  8. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Leonard Chamuriho kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.
    Mhandisi Chamuriho ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi, pia ameteuliwa na Mhe. Rais Magufuli kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  9. Rais Magufuli amemteua Prof. Adolf Faustine Mkenda kuwa Waziri wa Kilimo.
  10. Rais Magufuli amemteua Doto Mashaka Biteko kuwa Waziri wa Madini.
  11. Rais Magufuli amemteua Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
  12. Rais Magufuli amemteua George Boniface Taguluvala Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
  13. Rais Magufuli amemteua Ummy Ally Mwalimu kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
  14. Rais Magufuli amemteua Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Tayari Rais Magufuli alishawateua na kuwaapisha Mawaziri 2 ambao ni Dkt. Philip Isdor Mpango – Waziri wa Fedha na Mipango na Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi – Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Naibu Mawaziri walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

  1. Rais Magufuli amemteua Kigahe Exaud Silaoneka kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.
  2. Rais Magufuli amemteua Dkt. Angelina Sylvester Lubala Mabula kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
  3. Rais Magufuli amemteua Patrobas Paschal Katambi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira).
  4. Rais Magufuli amemteua Khamis Hamza Khamis kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
  5. Rais Magufuli amemteua Mwanaidi Ali Khamis kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.
  6. Rais Magufuli amemteua Kipanga Juma Omary kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
  7. Rais Magufuli amemteua Dkt. Festo Stephen Dugange kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).
  8. Rais Magufuli amemteua Byabato Stephen Lujwahuka kuwa Naibu Waziri wa Nishati.
  9. Rais Magufuli amemteua John Deogratius Ndejembi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).
  10. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Kundo Andrea Mathew kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
  11. Rais Magufuli amemteua Pauline Philipo kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
  12. Rais Magufuli amemteua Ndulane Francis Kumba kuwa Naibu Waziri wa Madini.
  13. Rais Magufuli amemteua Msongwe Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.
  14. Rais Magufuli amemteua Ummy Hamis Nderinanga kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu).
  15. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Marryprisca Winfred Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Maji.
  16. Rais Magufuli amemteua Abdallah Hamis Ulega kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  17. Rais Magufuli amemteua Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
  18. Rais Magufuli amemteua William Tate Ole Nasha kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  19. Rais Magufuli amemteua Marry Francis Masanja kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
  20. Rais Magufuli amemteua David Ernest Silinde kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).
  21. Rais Magufuli amemteua Hussein Mohamed Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.
  22. Rais Magufuli amemteua Dkt. Godwin Oloyce Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
  23. Rais Magufuli amemteua Geophrey Mizengo Pinda kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.

Wateule wote wataapishwa wiki ijayo Jijini Dodoma kwa tarehe na muda utakaotangazwa baadaye.

Send this to a friend