Orodha ya Mawaziri Vivuli wa ACT-Wazalendo walioteuliwa kuisimamia serikali

0
47

Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametangaza Wasemaji wa Kisekta 24 (Baraza Kivuli la Mawaziri) watakaokuwa na jukumu la kuisimamia Serikali kwa kuhakikisha changamoto zizonazowakabili wananchi zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Pamoja na mambo mengine baraza hilo limezingatia usawa wa kijinsia kwa kuwa na wasemaji 12 kutoka kila upande (wanaume na wanawake).

Dorothy Semu ameteuliwa kuwa Waziri Mku, akiwa ndiye mtendaji mkuu wa shughuli zote zitakazofanywa na Baraza hilo litakalokuwa linafanya shughuli zake nje ya bunge kuona Serikali inatekeleza wajibu wake.

Wateule wengine ni:
2. Abdul Nondo (Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Msemaji Mkuu wa Baraza Kivuli)

3. Emanuel Mvula (Wizara ya Fedha na Uchumi)

4. Fatma Fereji (Mambo ya Nje),

5. Masoud Salim (Wizara ya Ulinzi)

6. Mbarala Maharagande (Wizara ya Mambo ya Ndani).

7. Riziki Mngwali (Wizara ya Elimu)

8. Dkt. Nasra Omar (Wizara ya Afya)

9. Mwanaisha Mndeme (Wizara ya Uwekezaji, Mashirika ya umma na Hifadhi ya Jamii)

10. Pavu Abdallah (Utumishi wa Umma, Utawala Bora na Muungano)

11. Kulthum Mchuchuli (Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini)

12. Isihaka Mchinjita (Wizara ya Nishati),

13. Edgar Mkosamali (Wizara ya Madini),

14. Halima Nabalang’anya (Wizara ya Viwanda na Maendeleo ya Biashara),

15. Esther Thomas (Wizara ya Maji na Mazingira)

16. Wakili Victor Kweka (Waziri wa Katiba na Sheria)

17. Mtutura Mtutura (Wizara ya Kilimo Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi)

18. Bonifasia Mapunda (Ardhi na Maendeleo ya Makazi)

19. Injinia Mohammed Mtambo (Miundombinu ya Ujenzi Barabara na Reli)

20. Ally Saleh Alberto (Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Uchukuzi).

21. Juliana Makan’gwali (Wizara ya Maliasili na Utalii)

22. Wakazi Wasira (Utamaduni, Sanaa, Ubunifu na Michezo)

23. Mwalimu Macheyeki (Vijana, Kazi na Ajira)

24. Janeth Rithe (Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto).