Orodha ya nchi 10 za Afrika zenye mamilionea wa dola wengi zaidi; 

0
52

Kulingana na Ripoti ya Utajiri ya Afrika ya 2023 (Africa Wealth Report) iliyochapishwa hivi karibuni  kwa ushirikiano na New World Wealth, idadi ya mamilionea Afrika inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 42 katika miaka 10 ijayo.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa soko la utajiri la ‘Big 5’ barani Afrika, ambalo ni Afrika Kusini, Misri, Nigeria, Kenya, na Morocco, kwa pamoja ni asilimia 56 ya watu wenye thamani kubwa barani humo (HNWIs) na zaidi ya asilimia 90 ya mabilionea wake.

Kufikia sasa, bara hili lina HNWI (watu wenye utajiri kuanzia dola milioni 1) 138,000 pamoja na mamilionea 328 wenye thamani ya dola milioni 100 au zaidi, na mabilionea 23 wa dola za Kimarekani.

Afrika Kusini bado ina HNWIs mara mbili ya nchi nyingine yoyote ya Afrika na inachangia asilimia 30 ya mamilionea wa bara hilo.

Hii ni orodha ya nchi 10 za Afrika zenye mamilionea wengi zaidi;

1. Afrika Kusini (37,800)

2. Misri (16,100)

3. Nigeria (9,800)

4. Kenya (7,700)

5. Morocco (5,800)

6. Mauritius (4,900)

7. Algeria (2,800)

8. Ethiopia (2,700)

9. Ghana (2,600)

10. Tanzania (2,400)

 

Chanzo: Africa Wealth Report 2023

Send this to a friend