Katika baadhi ya maeneo ya Afrika, watu wanakabiliwa na ukosefu wa makazi kutokana na sababu kadhaa. Kuna nchi ambazo zinakumbwa na mapigano ya silaha na vurugu za ndani, na hivyo kuwalazimisha watu kuhama makazi yao kwa sababu ya usalama wao.
Pia, kuna sababu za kiuchumi zinazochochea watu kuishi mitaani au katika makazi duni. Ukosefu wa ajira na umaskini zinaweza kuwa sababu kubwa ya watu kuwa bila makazi.
Makazi duni na mazingira magumu katika baadhi ya maeneo, huchangia pia kuongezeka kwa watu wasio na makazi. Hii inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa, uhalifu, na hali ngumu ya maisha kwa watu hao.
Nchi 10 za Afrika zinazoongoza kwa ndoa za wake wengi
Tatizo la watu wasio na makazi ni changamoto kubwa ulimwenguni, lakini juhudi za pamoja zinaweza kusaidia kupunguza hali hii inayowaathiri watu wengi katika Afrika.
Hapa ni orodha ya nchi 10 za Afrika zenye viwango vya juu vya watu wasio na makazi kwa mwaka 2023, kulingana na data kutoka World Population Review;
1. Nigeria: Milioni 24.4
2. Misri: Milioni 12
3. DR Congo: Milioni 5.3
4. Somalia: Milioni 2.9
5. Sudan: Milioni 2.73
6. Ethiopia: Milioni 2.7
7. Sudan Kusini: Milioni 1.54
8. Cameroon: Milioni 1.03
9. Mozambique: 769,000
10. Burkinafaso: 700,000