Orodha ya nchi 10 zenye amani zaidi Afrika

0
229

Amani ni hali ya utulivu, usalama na kutokuwepo kwa migogoro au vurugu katika jamii au taifa. Ni msingi muhimu wa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Pasipo amani, shughuli za kila siku kama biashara, elimu, huduma za afya na usafiri huwa ngumu au haziwezekani kabisa.

Ingawa Afrika imepitia vipindi vya migogoro, vita vya wenyewe kwa wenyewe, na ukosefu wa utulivu katika baadhi ya nchi, bado kuna jitihada kubwa zinazofanywa na mataifa ya Afrika, jumuiya za kikanda kama Jumuiya ya Afrika (AU), ECOWAS, EAC, na mashirika ya kimataifa kuhakikisha bara linaendelea kuwa na amani endelevu.

Kwa upande wa Tanzania, imetajwa kuwa nchi yenye amani zaidi Afrika Mashariki, ikiwa nafasi ya 73 kati ya 163 duniani na nchi ya tisa barani Afrika.

Hizi ni nchi 10 zenye amani zaidi barani Afrika kwa mujibu wa ripoti ya Global Peace Index (GPI) mwaka 2025;

  1. Mauritius
  2. Namibia
  3. The Gambia
  4. Ghana
  5. Zambia
  6. Senegal
  7. Liberia
  8. Malawi
  9. Tanzania
  10. Angola