Orodha ya nchi 10 zenye rekodi mbaya zaidi ya Haki za Binadamu

0
79

Taasisi ya kuangazi haki za biabdamu (UN Watch) imetoa orodha ya nchi 10 ambazo zimeongoza kwa ukiukwaji mkubwa zaidi ya haki za binadamu duniani kote kwa mwaka 2020.

Katika orodha hiyo nchi mbili zinatoka barani Afrika, huku nyingi zikiwa za Ulaya na Asia.

10. Urusi
Matukio makubwa ni kiongozi wa upinzani Alexei Navalny kupewa sumu, ilikuwa na wafungwa wa kisiasa 362 huku wengine wakiteswa pamoja na Mashahidi wa Yehova 300. Shule, hospitali na masoko nchini zilipigwa mabomu, na ilimuunga mkono diktetea wa Belarus, Lukashenko.

9. Korea Kaskazini
Nchi hii ilimuua nahodha wa meli ya uvuvi kwa kusikiliza redio ya kimataifa akiwa baharini, ilipuuzia baa la njaa lililosababisha mamilioni kukosa chakula, iliwashikiliwa watu 100,000 kwenye kambi mbalimbali ambapo walikuwa wakifanyishwa kazi kwa nguvu, kuuawa, kulazimisha watoto kushuhudia watu wakiuawa.

8. Uturuki
Mwanaharakati wa haki za kibinadamu, Osman Kavala alifunguwa kwa makosa ya kochanga, mwanahabari Can Dundar alihukumiwa miaka 27 jela kwa makosa ya uongo ya ugaidi, Wakurd 460,000 walikatiwa huduma ya maji, ilishika nafasi ya kwanza kwa nchi iliyowafunga waandishi wa habari wengi, ilichochea vita Syria na Libya.

7. Cuba
Alidhibiti haki zote za msingi za binadamu, mwanamuziki Denis Solis alikamatwa kwa wimbo uliokosoa polisi, waandamanaji walisambaratishwa, mitandao ya kijamii ilifungwa kudhibiti habari zinazokosoa serikali, kulinda usafirishaji dawa za kulevya, ilizuia msaada wa chakula na dawa, iliwapeleka madaktari nje ya nchi kama adhabu.

6. Zimbabwe
Mwanahabari wa kiuchunguzi Hopewell Chin’ono alikamatwa baada ya kufichua siri ya rushwa kwenye wizara ya afya, iliwashughulikia na kuwateka waandamanaji na wakosoaji wa serikali, utekaji na unyanyasaji wa kijinsia, wauguzi na walimu walipigwa na kudhalilishwa kwa kukosoa mapambano dhidi ya UVIKO-19.

5. Saudi Arabia
Mtetezi wa haki za wanawake, Loujain al-Hathloul alifungwa miaka 6, mtetezi wa haki za binadamu Raif Badawi ameendelea kuwa gerezani baada ya miaka 8, iliweka zuio la kusafiri kudhibiti wakosoaji, ilipiga bomu shule, hospitali ya Yemen na kuua maelfu ya watu.

4. Venezuela
Ilivamia na kutaifisha mali za taasisi ambayo hutoa chakula kwa watoto wasio na uwezo, mkosoaji wa Maduro aliuawa, kiongozi wa upinzani alifukuzwa nchini humo, ilifanya uchaguzi batili, ilipuuzia majanga ya kibindamu yaliyozalisha wakimbizi milioni 5.

3. Cameroon
Ilimtesa hadi kufa mwandishi wa habari Samuel Abuwe, iliua watoto katika shule zinazozungumza Kiingereza ikiwa ni sehemu ya mgogoro wa Anglophone (watu 3,000 walifariki na 500,000 wamekimbia makazi tangu 2016), imetishia kuwaua viongozi wa upinzani
na imeghubikwa na unyanyasaji wa kijinsia.

2. Iran
Ilimuua Navid Afkari na mwandishi Ruhollah Zam kwa kukosoa serikali, ilifadhili mauaji ya Syria na mashambulio ya Hezbollah, iliwakamata wanawake kwa kutofunika nywele zao, ilitungua ndege ya abiria na kuua watu 176 na kudanganya kuhusu tukio hilo, iliwaua waliokuwa wakiandamana kwa amani.

1. China
Iliwaweka katika kambi watu milioni 1 wa jamii ya Uighurs, ilimfunga mtetezi wa haki za binadamu, shambaratisha Tibet, iliwanyamazisha waliotoa taarifa za awali za virusi vya korona kama Dkt. Li Wenliang na mwandishi Zhang Zhan, imedhibiti uhuru katika eneo la Hong-Kong.

Send this to a friend