Orodha ya nchi 5 Afrika zinazokabiliwa na njaa kali 2022

0
35

Shirika la misaada duniani kote la Ireland Concern na Shirika la Ujerumani la Welthungerhilfe hivi karibuni limetoa ripoti ya orodha ya nchi zinazokabiliwa na njaa kali zaidi barani Afrika 2022.

5. Niger
Kwa sasa Niger imeathiriwa na mzozo mbaya zaidi wa usalama wa chakula katika muongo huu, huku watu milioni 4.4 wakihitaji msaada wa haraka wa kibinadamu. Mgogoro huu uko katika muktadha wa kuendelea kuzorota kwa usalama katika eneo la Sahel, jambo ambalo linazidisha udhaifu wa kijamii na kiuchumi.

4. Chad
Tamko la dharura lilitolewa tarehe 1 Juni na Serikali ya Chad. Hii ni kutokana na hali mbaya ya sasa ya uhaba wa chakula na utapiamlo, ambayo itasababisha watu milioni 2.1 kuwa katika uhaba mkubwa wa chakula.

3. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban watu milioni 27 wanakabiliwa na uhaba wa chakula. Umoja wa Mataifa unatabiri kuwa huenda hali ikawa mbaya zaidi kutokana na mapigano ya hivi majuzi kati ya kundi la waasi la M23 na jeshi Mashariki mwa nchi hiyo.

2. Madagascar
Madagascar inakabiliwa na majanga mengi ya kibinadamu yanayoathiri watu milioni 9. Mvua zilizoshindwa kunyesha na ukame wa muda mrefu kusini mwa Madagascar vimesababisha watu milioni 1.5 kukosa chakula. Inakadiriwa watoto 500,000 walio chini ya miaka 5 watakuwa na utapiamlo, na 110,000 watakuwa na utapiamlo mbaya zaidi. Hatua za haraka zinahitajika kushughulikia mzozo wa lishe.

1.Jamhuri ya Afrika ya Kati
Takriban asilimia 79 ya watu milioni 4.7 nchini humo wanakadiriwa kuishi katika umaskini. Karibu watu milioni 3 wanaoishi katika C.A.R. wanahitaji msaada wa kibinadamu. Uzalishaji mdogo, masoko hafifu na kukosekana kwa usawa wa kijinsia yote ni sababu zinazochangia, pamoja na migogoro ya kisiasa na ukosefu wa usalama ambao unawakumba zaidi wanawake katika jamii za vijijini.

Chanzo: Business Insider Africa.