Orodha ya wachezaij bora wa ligi kuu Tanzania mwaka 2013-2023

0
111

Ligi Kuu ya Tanzania ni mashindano ya ngazi ya juu ya soka, na ni mojawapo ya ligi zinazopendwa sana na mashabiki. Vilabu kutoka maeneo mbalimbali hushiriki katika ligi hii na kila mwaka, timu hufanya michezo ya nyumbani na ugenini kushindania ubingwa.

Hii ni orodha ya wachezaij bora wa ligi kuu nchini Tanzania kuanzia mwaka 2013-2023;

2013/2014
Kipré Tchétché kutoka Ivory Coast alinyakua Tuzo ya Mchezaji Bora msimu wa mwaka 2013/2014 akitokea Azam FC.

2014/2015
Mchezaji Simon Msuva aliibuka kidedea baada ya kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu 2014/2015 akiwa klabu ya Young Africans.

2015/2016
Juma Abdul alifanikiwa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu kwa msimu wa 2015/2016 akiichezea Young Africans.

2016/2017
Mohamed Hussein “Zimbwe Jr” alinyakua Tuzo ya mchezaji bora wa msimu 2016/2017 kwa kikosi cha Simba.

2017/2018
John Bocco kutoka klabu ya Simba alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu

2018/2019
Meddie Kagere kutoka Rwanda alinyakuwa Tuzo ya Mchezaji Bora na Mfungaji Bora wa mwaka 2018/2019.

2019/2020
Mchezaji kutoka Zambia, Clatous Chama alishinda tuzo ya Mchezaji Bora kwa msimu wa 2019/20.

2020/2021
Nahodha wa Simba John Bocco alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/2021.

2021/2022
Aliyekuwa kiungo wa Yanga, Yanick Bangala kutoka DR Congo alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa ligi kuu Tanzania Bara.

2022/2023
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi ya NBC msimu wa mwaka 2022/2023 ilikwenda kwa mshambuliaji kutoka DR Congo, Fiston Mayele.