Orodha ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2021

0
63

Wanafunzi 759,706 (91.1%) kati ya wanafunzi 759,737 wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2021.

Taarifa hiyo imetolewa leo Disemba 17, 2020 na Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo.

Orodha ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2021

Kati ya waliochaguliwa, wavulana ni 368,174 na wasichana ni 391,532. Wanafunzi 4,169 watajiunga na shule za bweni, wanafunzi 970 watajiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi.

Aidha, amesema wanafunzi 1,238 watajiunga na shule za ufundi na wanafunzi 1,961 watajiunga na shule za bweni za kawaida.

Wanafunzi 74,166 hawajapangiwa shule katika awamu ya kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa, lakini amewatoa hofu na kusema kuwa watapangiwa shule katika awamu ya pili kabla ya Februari 28 mwaka 2021.

Send this to a friend