P2 inavyosababisha madhara kwenye hedhi na mifupa

0
15

Serikali imewataka wananchi na viongozi kwa ujumla kuhamasisha matumizi sahihi ya P2 kwa wasichana yanayozingatia ushauri wa wataalam ili kuepuka madhara yanayosababishwa na dawa hizo.

Akizungumza bungeni wakati akijibu maswali ya wabunge, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema matatizo yanayoweza kutokana na P2 endapo ikitumika hovyo ni pamoja na kupata hedhi isiyo na mpangilio na wakati mwingine kupata matatizo ya mifupa.

Aidha, akijibu kuhusu kuruhusu matumizi ya Sayana Press kwa wanawake katika vituo vya afya, amesema dawa hiyo ikitumika hovyo italeta madhara zaidi kuliko madhara ya P2.

Hata hivyo, Dkt. Mollel ameongeza kuwa Sayana Press imesajiliwa na TMDA na inapatikana kwenye vituo binafsi vya kutolea huduma za afya kwa wateja wanaohitaji.

“Sayana Press ukiiruhusu hovyo hovyo ndo tunaingia kwenye matatizo sawa na P2. Ndo maana tumesema hii watu wanaweza kuitumia kujidunga, ina madhara mengi pamoja na kupata maambukizi yasiyotarajiwa lakini kukutana na madhara makubwa kuliko hata haya ya P2.

Kwahiyo, tunasisitiza hiyo Depal ambayo wataenda hospitali na nesi anamchoma sindano kwa kufuata utaratibu ambao utalinda afya za watu wetu,” amesema.

Send this to a friend