Padri aliyetuhumiwa kubaka mtoto wa miaka 12 ashinda kesi

0
47

Mahakama mkoani Kilimanjaro imetupilia mbali shitaka linalomhusu Paroko wa Parokia teule ya Mtakatifu Dionis Arobagita ya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, Padri Sosthenes Bahati maarufu Soka (42) baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shitaka la kumbaka mtoto wenye umri wa miaka 12.

Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu Mkazi, Jenipher Edward ambapo inamfanya padri huyo ambaye kwa sasa amesimamishwa kutoa huduma zote za kipaimara kubakiwa na kesi mbili za tuhuma za kubaka watoto wa mafundisho ya kipaimara, matukio yanayodaiwa kutendeka kwa nyakati tofauti.

Hoja nyingine ambayo imezingatiwa ni kwamba ushahidi wa mwathirika (mtoto) umeibua mashaka juu ya ukweli wa kile alichoongea mahakamani kutokana na kutofautiana na mashahidi wengine.

Mchungaji aamriwa kumrudishia muumini fedha alizodai ni fungu la 10

“Lakini pia upande wa utetezi uliibua hoja ya mshtakiwa kutokuwepo eneo la tukio katika tarehe husika ambayo ni Agosti 26, 2022 ambapo walitoa notisi juu ya hilo na kuleta mashahidi wa kuthibitisha,” amesema.

Hakimu ameongeza kuwa kwa upande wa mashtaka pia ulishindwa kuleta mashahidi muhimu wa kuthibitisha kama tarehe hizo mshtakiwa alikuwepo eneo la tukio na kama kweli muathirika naye alikuwepo.

Send this to a friend