Panya Road wavamia na kujeruhi wakazi wa Bunju

0
38

Inaelezwa kuwa uhalifu unaofanywa na vijana maarufu ‘Panya Road’ bado unaendelea, hiyo ni baada ya wakazi wa Bunju B Mtaa wa Idara ya Maji kuvamiwa na kujeruhiwa na vijana wanaokadiriwa kuwa zaidi ya nane usiku wa kuamkia leo Februari 10, 2023.

Akizungumza na Mwananchi Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanne kufuatia tukio hilo ambao walifika eneo hilo na kuanza kupiga kelele za mwizi ikiwa ni njia ya kufanya uhalifu ambapo nyumba zilizotoka nje wakidhani kuna wezi walivamiwa na kushambuliwa.

“Kwa wale waliofungua walijeruhiwa huku wakiwaamuru watoe fedha na wale wasiotoa walijeruhiwa maeneo mbalimbali ya na kusababisha watu nane kupata majeraha ambapo waliikimbizwa hospitalini,” amesema.

Kamanda Muliro amebainisha kuwa pamoja na watu kujeruhiwa vijana hao walisababisha uharibifu ikiwemo kupasua runinga kwa watu wasiokuwa na fedha kisha walipanda bajaji na kukimbia  na ndipo walipokimbizwa na pikipiki.

Mwanamke afariki kanisani alipopelekwa kuombewa

“Walipofika njiani waliruka na kukimbia, polisi walifika na kuanza msako ambapo vijana wanne walikamatwa, ingawa wawili walijeruhiwa vibaya,” ameongeza

Aidha, Kamanda amesema kuwa baada ya kufanya upepelezi wa awali wamegundua wahalifu hao wametokea mkoani Pwani.

Send this to a friend