Papa Benedict XVI afariki Dunia

0
36

Papa Benedict XVI (95) amefariki dunia katika makazi yake Vatican, ikiwa ni takribani muongo mmoja tangu ajiuzulu nafasi hiyo kutokana na sababu za kiafya.

Papa Benedict aliongoza Kanisa Katoliki kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2013, na kuwa kiongozi wa kwanza kujiuzulu ndani ya miaka 600, tangu alipojiuzulu Gregory XII mwaka 1415.

Ikitangaza kifo hicho Vatican imesema “Kwa masikitiko ninawajulisha kuwa Papa Mstaafu, Benedict XVI, amefariki dunia leo saa 9:34 katika Monasteri ya Mater Ecclesiae huko Vatican.”

Hivi karibuni Papa Francis alitoa wito kwa hadhira yake ya mwisho ya mwaka huko Vatican kusali sala maalum kwa ajili ya Papa Benedict ambaye alisema alikuwa mgonjwa sana.

Send this to a friend