Papa Francis awaonya makasisi na watawa wanaotazama video za ngono

0
38

Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amekiri kuwa makasisi na watawa pia hutazama video za ngono mtandaoni huku akionya kuwa tabia hiyo inadhoofisha moyo wa kipadri.

Ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali kuhusu jinsi vyombo vya habari vya kidijitali na mitandao ya kijamii vinapaswa kutumiwa, katika kikao kilichofanyika makao makuu ya kanisa hilo huko Vatican.

Wapenzi wengi chanzo cha upungufu wa nguvu za kiume

“Ponografia, ni tabia ambayo imewaambukiza watu wengi, hata makasisi na watawa. Ibilisi huingia kutoka huko,” aliwaambia makasisi na waseminari.

Papa amefafanua kuwa kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii na ulimwengu wa kidijitali, ni lazima zitumike lakini akawasihi wasipoteze muda wao mwingi kuzitumia.

“Moyo safi, ambao unapokea Yesu Kristo kila siku, hauwezi kupokea habari hizi za ngono,”ameeleza.

Ameshauri kikundi cha viongozi hao wa kidini kufuta programu hizo kutoka kwenye simu zao, ili kuepuka pia kupata majaribu na kufanya vitendo visivyofaa vya kimaadili.

Send this to a friend