Parimatch yawakutanisha Simba na Yanga

0
38

Zikiwa zimesalia raundi chache kufikia tamati kwa michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Kampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch imetoa zawadi ya tiketi za VIP A pamoja na jezi kwa washindi watano ambao ni mashabiki wa Simba na Yanga kwenda kutazama mtanange wa watani wa jadi ambao unachezwa leo katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

Hayo yamewekwa wazi na Afisa Habari wa Parimatch Tanzania Bwana Ismael Mohamed wakati alipokuwa akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi zawadi hizo kutoka katika droo ya shindano ya Dar Derby

Aidha, Ismael amewataja washindi hao kuwa ni John Haroldy, Collin Frank, Golingo Yegella, Clay Kennedy pamoja na Baraka Kimaro ambao wote wametokea maeneo tofauti tofauti ya jiji la Dar es Salaam.

“Kutokana na ukubwa wa mechi hizi za Simba na Yanga, sisi kama Parimatch tumeona ni vyema wateja wetu wakapata fursa ya kwenda kushuhudia Live mtanange huu wa kukata na shoka wakiwa dimbani pale na hii haitoishia kwenye Darby hii, tumejipanga kufanya makubwa katika Darby zote zitakazochezwa katika ligi ya NBC” alisema Ismael.

Kwa upande wao mashabiki hao kwa ujumla wamedai kuwa wamejisikia furaha kuona Parimatch inathamini wateja wao na kuwapa kile kilichobora nyakati zote pindi wanapokuwa wanahitaji.

Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya 100% mpaka TZs 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nasi! Parimatch imekuwepo nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual.

Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.

Send this to a friend