Pasipoti 10 za nchi za Afrika zenye nguvu zaidi duniani

0
63

Henley Passport Index hutoa orodha ya uimara wa pasipoti duniani kwa kuangalia idadi ya nchi ambazo mmiliki wa paspoti husika anaweza kuingia bila kuhitaji visa. Takwimu hizo zinatokana na taarifa kutoka International Air Transport Association (IATA).

Orodha hiyo inajumuisha pasipoti 199 na vituo 227 vya kusafiri. Orodha hii hutoka kila robo ya mwaka, na huchukuliwa kama kiwango sahihi cha kupima uimara wa pasipoti.

Duniani kote pasipoti ya Japan ndiyo inayoongoza ambapo inamwezesha mwenye nayo kuingia katika nchi 192 bila kuhitaji malipo ya visa.

Kwa upande wa Afrika, hapa chini ni orodha ya pasipoti 10 zenye nguvu zaidi Afrika:

1. Shelisheli
Hii ni ya kwanza Afrika na 29 ya duniani. Mmiliki wa pasipoti hii anaweza kuingia katika nchi 156 pasi na kuhitaji visa.

2. Botswana
Wakati ikiwa ya pili Afrika, duniani inashika nafasi 67 na mmiliki wake anaweza kuingia katika nchi 67 bila kuhitaji kulipia visa.

3. Namibia
Duniani ipo nafasi ya 73 na mmiliki wake anaweza kuingia katika 78 tofauti bila visa.

4. Lesotho
Inashika nafasi 74 duniani na mwenye nayo anaweza kuingia katika nchi 77.

5. Malawi
Afrika ni ya 5 huku duniani ikiwa katika nafasi ya 76. pasipoti ni ufunguo wa kuingia katika 73 bila visa.

6. Kenya na Tanzania
Pasipoti za nchi hizi mbili za Afrika Mashariki zimeshika nafasi ya 77 duniani. Yeyote mwenye pasipoti ya nchi hizi ataweza kuingia katika nchi 72 duniani bila visa

7. Tunisia na Zambia
Zote mbili zimeshika nafasi ya 78 zikiwa ni funguo za kuingia katika nchi 71 kwa kila moja

8. Gambia
Duniani ipo katika nafasi ya 80, na inatoa fursa kwa mwenye nayo kuingia katika nchi 68.

9. Uganda
Kutoka Afrika Mashariki, pasipoti yake imeshika nafasi ya 81 duniani, ikiwa na uwezo wa kukufungulia milango ya 67.

10. Cape Verde
Hii inafunga orodha ikiwa nafasi ya 82 duniani ikiwa na uwezo wa kukuwezesha kuingia katika nchi 66 bila viza.

Send this to a friend