Pasipoti ya Tanzania yapanda nafasi saba kwa uimara duniani

0
38

Pasipoti ya Tanzania imepanda nafasi saba katika viwango vya ubora vya Henley kwa mwaka 2023 ikishikilia nafasi ya 69 kati ya pasipoti zenye nguvu zaidi duniani kutoka nafasi ya 76 mwaka 2022.

Kutokana na nafasi hiyo, mmiliki wa pasipoti hiyo sasa anaweza kuingia katika nchi 73 bila kuhitaji visa.

Viwango hivyo ambavyo vinategemea data kutoka Shirikisho la Kimataifa la Usafiri wa Anga (IATA), inaonesha kuwa Singapore kwa sasa ndio inashikilia taji la pasipoti yenye nguvu zaidi duniani. Wananchi wa Singapore wanaweza kutembelea maeneo 192 kati ya 227 ulimwenguni bila ya kuhitaji visa.

Ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Tanzania inashika nafasi ya pili nyuma ya Kenya, ambayo inashika nafasi ya 67 yenye uwezo wa kusafiri kwenda nchi 77 bila visa, huku Malawi ikishikilia nafasi ya 68 ambapo wamiliki wa pasipoti watasafiri nchi 75 bila visa.

Spika Dkt. Tulia njia nyeupe Urais IPU, Afrika yamuunga mkono

Katika bara la Afrika, Afrika Kusini inajivunia pasipoti yenye nguvu zaidi, ikishikilia nafasi ya 51 kimataifa ambapo inaweza kukusaidia kuingia nchi 106. Botswana inafuata kwa nafasi ya 58, ikiwaruhusu wamiliki wa pasipoti yake kufika nchi 89 bila visa, wakati Namibia inashika nafasi ya 62, ikitoa ufikiaji wa visa bila malipo kwa nchi 81.

Send this to a friend