Paul Makonda aongezewa mashitaka

0
39

Mawakili wa mwandishi wa habari, Said Kubenea wamewasilisha upya mahakamani maombi yaliyofanyiwa marekebisho ya kushitaki ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mawakili hao wamewasilisha upya maombi hayo baada ya kuondoa maombi ya awali kutokana na kuwa na kasoro mbalimbali ambazo zimeelezwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinodnoni na Wakili wa Serikali, Daisy Makakala.

Isome hapa hati ya mashitaka yanayomkabili Paul Makonda

Kiongozi wa jopo la mawakili wa Kubenea, Hekima Mwasipo amedai hati ya awali ilikuwa na kasoro mbalimbali hasa za kiuandishi, mfano kukosewa kwa jina la mshitakiwa wa tatu, na pia wamebadili ili kuongeza mashitaka ambayo awali hayakuwepo kwenye maombi.

Kasoro nyingine iliyojitokeza baada ya kuibuliwa na Wakili Makakala ni majina ya mwasilisha maombi na aliyeapa kuwa tofauti, na baadaye kukubaliana na maombi ya mawakili wa upande wa Kubenea.

Makonda: Mapenzi ya Mungu ni makubwa kuliko mapenzi yangu

Kubenea anazishitaki ofisi ya DPP na DCI kwa madai ya kushindwa kuchukua hatua dhidi ya mshitakiwa wa tatu, Paul Makonda kwa makosa anayodaiwa kuyatenda.

Hata hivyo mawakili hao hawakutaja makosa mapya ambayo wameyaongeza kwenye maombi yaliyowasilisha mahakamani leo.

Katika hati ya mashitaka ya awali miongoni mwa makosa yanayomkabili Makonda ni pamoja na matumizi mbaya ya madaraka, kuvamia ofisi za Clouds Media Group na kuingilia urusha matangazo wa chombo cha habari.

Send this to a friend