PDPC: Wanaofunga CCTV kamera maeneo ya faragha wanakiuka sheria

0
26

Tume ya Ulizi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imezionya taasisi na kampuni zote nchini zinazotumia kamera za usalama katika maeneo mbalimbali ya faragha ikieleza kuwa ni ukiukwaji wa sheria.

Katika taarifa iliyotolewa na PDPC imesema kumekuwa na taarifa za uwepo wa matukio ya kuwekwa kamera za usalama (CCTV) katika maeneo ya faragha kama vile vyooni na maeneo mengine ambapo ni kinyume na sheria ya ulinzi na taarifa binafsi.

“Taasisi na kampuni zote nchini zinakumbushwa kuzingatia kikamilifu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Na. 11,2022 na kanuni zake wakati wa kufunga mifumo ya usalama maeneo ya kazi au nyumbani. Ni muhimu hatua zozote za ufuatiliaji ziwe za uwiano na zenye kuheshimu haki za faragha za watu,” imeeleza taarifa.

Imeongeza kuwa faragha ya mhusika wa taarifa ni ya msingi na ni jukumu la kila taasisi kulinda taarifa binafsi za watu

Send this to a friend