Poda ya watoto ya J&J yadaiwa kusababisha saratani

0
24

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linachunguza uwezekano wa kuwepo sokoni poda za wawatoto zinazotengenezwa na kampuni kubwa ya dawa ya Marekani ya Johnson & Johnson (J&J) ambazo zinadaiwa kusababisha saratani.

Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Athuman Ngenya amesema tayari wameanza kukusanya sampuli za unga wa J&J kwa ajili ya uchunguzi mpya wa kimaabara.

“Baada ya kupata taarifa hizi, tulianzisha uchunguzi ili kubaini iwapo poda za talcum zinazozungumziwa zimeingia nchini ili tuchukue hatua stahiki,” alisema.

Kenya: Ugumu wa uchumi wasababisha mamilioni kukata tamaa ya kutafuta kazi

Hayo yanajiri baada ya J&J kupendekeza kiasi cha dola za Kimarekani 8.9 bilioni (TZS trilioni 21) kutatua kesi za miaka mingi zinazodai kuwa bidhaa zake zilisababisha saratani.

J&J imekuwa ikikabiliwa na maelfu ya kesi kuhusu poda ya talcum iliyo na chembechembe za asbesto inayodaiwa kusababisha saratani ya ovari, hata hivyo kampuni hiyo haijawahi kukiri makosa hayo, lakini iliacha kuuza poda hizo nchini Marekani na Kanada mnamo Mei 2020.

Send this to a friend