Polepole ateuliwa kuwa Balozi, Mchechu arejeshwa NHC

0
44

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

1. Amemteua Bwana Waziri Kindamba Waziri kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Bwana Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Mwita Rubirya ambaye amestaafu kwa umri.

2. Amemteua Bwana Humphrey Hezron Polepole kuwa Balozi wa Tanzania Nchi ya Jamhuri ya Malawi.

3. Amemteua Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 Ibara ya 67(2) (g) ikisomwa pamoja na Ibara ya 71(1)(a).

4. Amemteua Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (Mstaafu) Ernest Jumbe Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari (Tanzania Port Authority)

5. Amemteua Meja Jenerali John Julius Mbungo, Mkurugenzi Mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Meli Tanzania (MSCL).

6. Amemteua Bwana Peter Rudolph Ulanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Ulanga ni Mkurugenzi Mstaafu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF)

7. Amemteua Nehemia Kyando Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Mchechu aliwahi kutumikia Shirika la Nyumba (NHC) huko nyuma kwa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na anachukua nafasi ya Dkt. Maulid Banyani, atapangiwa kazi nyingine.

Kindamba na Balozi Mteule Polepole wataapishwa Machi 15, 2022 saa 04:00 asubuhi viwanja vya Ikulu, Chamwino, Dodoma.

Send this to a friend