Polepole: CHADEMA imemdhulumu TID kauli ya ‘Ni Yeye’

0
36

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamemzulumu mwanamuziki TID kwa kutumia kaulimbiu aliyoibuni ‘Ni Yeye’ bila kumshirikisha.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Humphrey Polepole ameeleza kuwa kitendo hicho hakikubali na kwamba Watanzania watakichukulia hatua chama hicho cha upinzani.

“Nampa pole TID sababu hawa majamaa ni mazulumati wametudhulumu wimbo wa Taifa. TID anapambana mtu wa watu ametengeneza Ni Yeye na ile ilikuwa Magufuli, wale majamaa wameichomeka kule. Hawajamshirikisha hawajamuomba kwa kweli sisi kama Watanzania tutawachukulia hatua,” ameeeleza Polepole.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa Rais Dkt. Magufuli ambaye ni mgombea wa CCM atachukua fomu ya uteuzi wa kugombea Urais wa Tanzania wiki hii jijini Dodoma, lakini hakutaja siku ya tukio hilo.

Aidha, amesema Agosti 15 mwaka huu chama hicho kitakutana na wasanii zaidi ya 109 pamoja na bendi katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya kutambulisha nyimbo zitakazotumika kabla, wakati na baada ya kampeni.

Send this to a friend