Polisi ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kubaka na kumuua daktari

0
1

Mahakama moja nchini India imemhukumu kifungo cha maisha Sanjay Roy, polisi aliyekuwa akijitolea katika Idara ya Polisi, baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na mauaji ya daktari katika Chuo na Hospitali ya Tiba ya R G Kar, mjini Kolkata.

Mwili wa daktari huyo, ambaye alikuwa bado kijana na katika hatua za mwanzo za taaluma yake, ulipatikana katika darasa la chuo mnamo Agosti 9, tukio lililochochea maandamano ya madaktari waliokataa kufanya kazi kwa wiki kadhaa, wakitaka haki na kuboreshwa kwa usalama katika hospitali za umma.

Hakimu Anirban Das, aliyetoa hukumu hiyo, amesema ushahidi wa mazingira umemtia hatiani Roy, licha ya mtuhumiwa huyo kudai kuwa alisingiziwa na kuomba msamaha.

Hata hivyo, polisi waliochunguza kesi hiyo, wamesisitiza kuwa ukatili wa tukio hilo ulikuwa wa kiwango cha juu kiasi kwamba Roy alistahili kupewa adhabu ya kifo. Hata hivyo, mahakama haikuridhika na ombi hilo.