Polisi Dar wapiga marufuku jogging siku za ibada

0
39

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa halitatoa vibali kwa ajili ya watu kufanya mbio za taratibu (jogging) katika siku za ibada kwa sababu wafanya mazoezi hao wamekuwa wakiwachelewesha waumini kwenda kwenye nyumba za ibada.

Kamanda Lazaro Mambosasa amesema kuwa waumini wengi Dar es Salaam hutumia magari kwenda kwenye nyumba za ibada, hivyo vikundi vya wakimbiaji huwachelewesha kwa kutumia njia ambazo waumini hao wanatumia.

“… unapoingiza jogging barabarani, unapoingiza maandamano barabarani ya aina yoyote ile yanapelekea kufunga barabara. Ibada zibakwenda na muda… Wanapopata vikwazo njiani wanajikuta wanashindwa kufika kwa wakati, wanakwenda wanakuta ibada zimeshaanza,” amesema Mambosasa.

Amesama siku za ibada zinafahamika kuwa ni Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, na hivyo hawatatoa vibali kwa siku hizo.

Vikundi mbalimbali vimekuwa vikifanya mazoezi ya pamoja kwa kukimbia pembezoni mwa barabara hasa mwishoni mwa juma.

Send this to a friend