Polisi Dar wasitisha kumhoji Tundu Lissu

0
40

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesitisha barua ya kumuita mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa amesema uamuzi huo umetokana na IGP Simon Sirro kumtaka mwanasiasa huyo kuripoti kituo cha polisi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mahojiano.

Tundu Lissu atakiwa kuripoti kituo cha polisi Kilimanjaro

Mwanasiasa huyo anadaiwa kukaripia maofisa wa polisi akiwa kwenye kampeni zake.