Polisi: Hakuna askari aliyechomwa moto Njombe

0
29

Jeshi la Polisi mkoani Njombe limekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoeleza kuhusu askari polisi mkoani humo kuchomwa moto na kuporwa silaha.

Polisi wamesema wanaendelea kumfuatilia mtu au watu waliotengeneza taarifa hiyo kwa kutumia picha mjongeo ya tukio la zamani ambalo askari walikwenda kutoa msaada kwa wananchi.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa “Jeshi la Polisi linatoa wito kwa baadhi ya wananchi wenye tabia za kuandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji kwa njia mbalimbali kuiacha kwani ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya Mtanzania na hakuna faida yoyote kwa wanaofanya hivyo pamoja na familia zao na kwa jamii kwa ujumla.”

Send this to a friend