Polisi: Hakuna mgomo wa malori mpaka wa Namanga
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewahakikishia wakazi wa mkoa huo kuwa hali ya usalama katika mpaka wa Namanga uliopo katika Wilaya ya Longido ni shwari.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Justine Masejo wakati alipotembelea mpaka huo kuona hali ya usalama kutokana na kuwepo kwa foleni kubwa ya malori yanayosubiri kufanyiwa ukaguzi.
Mifugo 314 yakamatwa kwa kuingizwa nchini kinyume na taratibu
Amesema hakuna mgomo wowote wa madereva, na kusisitiza kuwa hawatasita kuwachukulia hatua watu wachache ambao watajaribu kuvunja amani katika eneo hilo, kwani vyombo vya dola vipo makini wakati wote.
Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa mpaka huo, Audax Asheri amesema wanashirikiana na upande wa Kenya kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ili magari yapite vizuri na kuondoa foleni ambayo ipo katika mpaka huo.