Polisi: Hatumjui aliyevamia nyumbani kwa Polepole

0
43

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga amesema uchunguzi tukio la kuvamiwa nyumba ya Mbunge Humprey Polepole na kwamba uchunguzi unaendelea, na pia hawawezi kusema ni lini uhalifu huo ulifanyika.

Kupitia mitandao ya kijami Polepole ameeleza kwamba nyumba yake ilivamiwa na watu wasiojulikana ambao waliiba televisheni moja ya inchi 55 na spika.

“Upelelezi wenye kuambatana na msako mkali unaendelea ili kuwatafuta wahusika wa tukio hilo na kuwachukulia hatua za kisheria. Suala la kwamba ni habari ya siasa sisi hatuoni kwa sababu makazi yamevunjwa,” amesema Lyanga.

Amesema kwa sasa hawajui nia ya wahalifu hao kwa sababu hakuna ujumbe walioacha baada ya kumkosa mwenyeji ambaye ni Polepole aliyekuwa nje ya mkoa huo.

“Bado haieleweki ni lini hasa palivunjwa kwa hiyo si rahisi kujua kulikuwa na nia ya kutaka kumdhuru yeye kama yeye kwa sababu hakuna ujumbe wowote ambao tumeweza kuubaini kuwa umemtishia yeye maisha yake,” ameongeza.

Send this to a friend