Polisi: Kauli za Mwingira zinajenga chuki kati ya wananchi na serikali yao

0
41

Jeshi la Polisi limesema limefuatilia kwa karibu kauli zinazodaiwa kutolewa na Askofu wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira na kuona zinajenga chuki na hofu kwa wananchi dhidi ya serikali yao.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amesema hayo katika taarifa yake kwa umma  kuhusu kumhoji kiongozi huyo.

Muliro amesema jeshi hilo limeagiza ndani ya sas 24 kuanza kuhojiwa askofu huyo juu ya tuhuma mbalimbali alizotoa dhidi ya serikali ikiwemo  njama za maofisa wa serikali kutaka kumuua.

Ameeleza zaidi kwamba kwa uzito wa shutuma hizo ni lazima kiongozi huyo apatikane haraka iwezekanavyo na ahojiwe kwa kina juu ya kila kipengele ambacho jeshi litaona kuna viashiria vya vigezo vya kijinai.

Jeshi hilo limesema halitosita kumkamata na kumhoji mtu yeyote anayetumia vibaya uhuru wa kutoa maoni.

Send this to a friend